Triple A FM

Mwingine ajinyonga Arusha

29 January 2025, 11:21 am

Na Joel Headman, Arusha

Hali ya majonzi imezidi kutawala jijini Arusha kutokana na kuongezeka kwa vifo vya kujuinyonga.

Hii ni baada ya kijana mwenye umri wa miaka 32 mkazi wa kijiji cha Oldadai Elirehema Ernest kujinyonga kwa kile kinachodhaniwa ni ugomvi wa kimahusiano

Kinachofikirisha zaidi kwenye tukio hilo lililotokea asubuhi ya Januari 28,2025 ni aina ya kifo cha Elirehema Ernest na namna kilivyo tokea akidaiwa kuvalia gauni na viatu vya mpenzi wake kabla ya kujinyonga.

Akizungumza na Triple A fm baba mzazi wa Elirehema mzee Ernest Kivuyo ameeleza kuwa kijana wake mwenye miaka 32 alikuwa kwenye mahusiano ambayo hayakuwa rasmi na amejaribu mara kadhaa kuwashauri kuachana au kuyarasimisha japo hakufanikiwa.

Sauti ya baba mzazi wa Elirehema

Mwenyekiti wa kijiji cha Oldadai Lomayani Kivuyo ameeleza kuwa hakuna uhakika kuwa marehemu alikuwa ameachana na mpenzi wake kwani kulikuwapo mawasiliano baina ya binti huyo na mzazi wa Elirehema siku moja kabla ya kufariki kwake.

Sauti ya mwenyekiti wa Kijiji

Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kumkuta marehemu akiwa amevalia gauni na viatu maarufu kwa jina la Slipers vinavyodhaniwa kuwa vya mpenzi wake.

Shuhuda wa tukio

Majirani Bado tunafuatilia taarifa rasmi ya kiuchunguzi kutoka jeshi la polisi mkoani hapa kufahamu chanzo halisi cha kifo hicho