Triple A FM

Watoto Marufuku Sokoni

28 January 2025, 10:17 am

Wafanyabiashara katika soko kuu la Arusha

Na Joel Headman, Arusha

Uongozi wa soko kuu jiji la Arusha umepiga marufuku watoto kujihusisha na biashara sokoni hapo.

Katazo hilo limekuja ikiwa ni siku chache baada ya shule kufunguliwa kote nchini. Akizungumza na Triple A fm amesema kumekuwa na tabia ya wafanya biashara kuchukua watoto maeneo ya vijijini na kuwaleta sokoni hapo kwa lengo la kuwasaidia kuuza bidhaa zao kitu ambacho ni kinyume na sheria za nchi kwani wanasitisha masomo