Makonda; Diwani,Mbunge waburuzwe kwenye tope kama…
17 December 2024, 9:05 pm
Na Joel Headman Arusha
Siku 1 baada ya wananchi wa kata ya Muriet Jijini Arusha kumtembeza kwenye matope na maji machafu diwani wao Francis Mbise mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda ameeleza kufurahishwa na tukio hilo.
Akizungumza leo kwenye kongamano la 15 la wataalam wa ununuzi na ugavi linaloendelea jijini Arusha ambalo limezinduliwa na naibu waziri mkuu na waziri wa nishati dk.Doto Biteko, amewapongeza wananchi hao kwa kitendo hicho alichoeleza kitachochea uwajibikaji wa viongozi.
Tukio hilo la kipekee lililoteka hisia za wengi limetokea jana Dec 16 baada ya wananchi hao wa mtaa wa Kimara mwisho kudai kuwa diwani wao amewahadaa kwa muda wa miaka mitatu bila kutekeleza ahadi za kuwatengenezea miundombinu bora.
Wakizungumza na wanahabari huku mmoja wao akionekana kuogelea kwenye maji, wameeleza kuwa hali hiyo inahatarisha umoja wa familia kwani baadhi ya wanaume wamekuwa wakilala kusikojulikana kwa kusingizia mvua.
Kwa upande wa diwani huyo ameonekana kuwatuliza wananchi hao na kueleza kuwa mambo yatakuwa sawa.
Akizungumza mkuu wa wilaya Arusha Felician Mtahengerwa ameelekeza wawekezaji wanaochimba moram katika maeneo hayo kumwaga moram kwenye barabara hizo wakati maamuzi zaidi yakisubiriwa