Triple A FM

Tulitoa muda wa kutosha kwa wanahabari kujiendeleza kwa mujibu wa sheria-Serikali

13 May 2024, 11:42 am

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Habari Maelezo Bw. Mobhare Matinyi akizungumza na wanahabari jijini Arusha.Picha na Anthony Masai.

”Serikali ilitoa muda wa kutosha kwa wanahabari kujiendeleza ili kufikia kiwango cha elimu inayotambulika kisheria”

Na. Anthony Masai.

Serikali ipo katika hatua za mwisho kukamilisha mchakato wa kutangaza kanuni za sheria ya huduma ya vyombo vya habari ya mwaka 2016 na kuunda Bodi ya Ithibati ambayo pamoja na masuala mengine itawatambua wanahabari kwa viwango vyao vya elimu kuanzia ngazi ya Stashahada(Diploma).

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Habari Maelezo Bwana Mobhare Matinyi amesema hayo katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari,ambayo kwa mkoa wa Arusha yamefanyika Mei 11 mwaka huu.

Bwana Matinyi amesema Serikali ilitoa muda mrefu kwa wanahabari kujiendeleza na sasa wakati umefika kwa sharia hiyo kuanza kutekelezwa kwa ukamilifu kwani kanuni zipo tayari ambazo zitaongoza kuunda vyombo vingine ikiwemo baraza la Ithibati.

sauti ya mobhare matinyi

Kuhusu suala la mashahi duni ya wanahabari nchini na utata wa ajira zao,Bwana Matinyi amesema,maoni yaliyokusanywa na kamati iliyoundwa na Serikali kuhusu hali ya uchumi wa vyombo vya habari na wanahabari nchini;yanatarajiwa kuwasilishwa hivi karibuni ambapo yatatoa picha kamili na namna ya kushughulikia changamoto hizo.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya habari nchini JOWUTA Bw.Mussa Juma.

Awali Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa vyombo vya habari nchini JOWUTA Bwana Mussa Juma,alizungumzia suala la mikataba ya ajira kama changamoto kubwa ya wanahabari kupata maslahi yanayoenda na kazi zao.

sauti ya Mussa Juma.

Aidha amezungumzia utafiti kuhusu vipato vya wanahabari kwa nchi za Afrika Mashariki,Tanzania ikiwemo.

sauti ya Mussa Juma.
Mkurugenzi wa huduma za kijamii katika Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt Iren Isaka akitoa hotuba yake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani kwa Mkoa wa Arusha yaliyofanyika Mei11,2024

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo,Mkurugenzi wa Huduma za Jamii katika Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt.Irene Isaka ameahidi kuendeleza ushirikiano na Waandishi wa habari Mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla ili kuendelea kutangaza mambo mazuri ndani ya Jumuiya hiyo.

Aidha ameeleza kuwa, uhuru wa vyombo vya habari ni kuwajibika na kuandika habari zenye ukweli na uhakika kwa kufuata misingi na miiko ya Uandishi wa habari, pia kuheshimu haki na uhuru wa watu wengine.