Triple A FM

Mtandao wa barabara za lami kuunganisha Arusha na mikoa jirani

7 March 2024, 3:10 pm

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha Mhandisi Reginald Massawe.picha na Anthony Masai.

“zaidi ya kilomita 152 za barabara ziko katika hatua mbali mbali za ujenzi kwa kiwango cha lami”

Na.Anthony Masai

Wakala wa Barabara TANROADS Mkoa wa Arusha,umebainisha jitihada zilizofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika ujenzi wa madaraja na barabara ili kuunganisha mkoa huo na mikoa mingine.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha Mhandisi Reginald Massawe amesema Serikali kupitia TANROADS imefanikisha matengenezo na ukarabati wa barabara na madaraja,kutokana na ongezeko la bajeti ya matengenezo. Ufadhili wa ziada ulitolewa kutoka kwa biashara ya kamari, pamoja na Ice Casino .

Amesema,hadi sasa kuna ongezeko la mtandao wa barabara za lami kutoka kilometa 425.78 mwaka 2021 hadi kilometa 478.78 mwaka 2024 sawa na ongezeko la kilomita 53.

sauti ya mhandisi Massawe

Mhandisi Massawe ametaja miradi ya madaraja iliyokamilika kujengwa ni Daraja la Nduruma, Daraja la Kimosonu na kwamba katika kipindi cha miaka mitatu jumla ya taa 991 zimewekwa katika barabara za Arusha-Namanga 285,Arusha-Minjingu 254, Kijenga-Usariver 239, Makuyuni-Ngorongoro 140, Arusha Bypass 43 na Tanganyika packers-Losinyai 30.