Chande: Mabadiliko Posta lazima, dunia ya sasa ni kidijitali
19 January 2024, 6:44 pm
“kuhusu usafirishaji wa mizigo,tumeshafungua vituo vya utimilifu Arusha,Zanzibar,Dodoma na Dar es Salaam ili ndani ya siku mbili mtu akiwa sehemu yoyote duniani anapokea mzigo wake“
Na. Anthony Masai.
Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Maharage Chande amesema,hakuna namna ambavyo shirika hilo linaweza kuendelea na utaratibu wa utendaji kazi wake wa miaka 10 iliyopita,katika kipindi hiki cha maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia ambayo ni chachu ya mabadiliko yanayofanyika kwa sasa katika sekta ya mawasiliano na usafirishaji wa mizigo.
Amesema hayo jijini Arusha kwenye maadhimisho ya miaka 44 ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU), ambapo ameongeza kuwa shirika la posta Tanzania ,hivi sasa linafanya mabadiliko makubwa ya kuboresha huduma zake ili kuendana na kasi ya teknolojia ambayo inakua kwa kasi.
Sauti ya Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Maharage Chande.
Katika maadhimisho hayo,Waziri wa Habari, Mawasiliano Teknolojia na Posta wa Zimbabwe Dk.Tatenda Annastacia Mavetera ameutaka Umoja wa Posta Afrika kuweka mikakati thabiti ya kiutendaji ili kwenda na kasi ya mabadiliko ya kidijitali hali inayowezesha kuvuta zaidi wafanyabiashara kutumia huduma za posta.