Triple A FM

WAMACHINGA WATII SHERIA BILA SHURUTI ARUSHA.

8 November 2021, 2:02 pm

Wafanyabiashara ndogondogo wakibomoa vibanda vyao katika moja ya mitaa ya jijini Arusha.

Na.Sunday Douglas,Arusha.

Wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga ambao walikuwa wamejenga vibanda juu ya madaraja, kandokando mwa barabara na maeneo mengine ambayo sio rasmi jijini Arusha,leo wameanza kuhama.

Wamachinga hao wanahama kutokana na tangazo la Mkuu wa Mkoa Arusha, John Mongela na Mkurugenzi wa Jiji hilo, Dk John Pima lililowataarifu kuwa ikifika saa sita usiku kwa ambao watakuwa hawajaondoka kwa hiari ,vibanda vyao vitavunjwa.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella akisisitiza jambo wakati akiogea na baadhi ya wafanyabiashara jijini Arusha.

Bwana Mongela amesema tayari maeneo ya kuhamia machinga yamekamilika ambayo ni eneo la Kilombero, Soko la Mbauda, Soko la Kwamrombo, Makao Mapya, Engutoto na eneo la Ulezi.

Baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema wanaunga mkono jitihada za Serikali kuwapatia maeneo mbadala.

machinga wakizungumzia zoezi la kuhamishwa.

Hivi karibuni Mkurugenzi wa Jiji hilo, Dk John Pima alisema machinga wote waliosajiliwa katika maeneo yao ya awali watapata maeneo mapya.

mwisho.