Smile FM Radio
Smile FM Radio
18 November 2026, 4:56 pm

Pichani kutoka kulia ni Salma Amour Meneja TMA Manyara na kushoto ni Haji Hamimu, muangazi kutoka TMA Manyara (picha na Frank Kijukuu)
Kateshi ambapo nyumba takribani 32 ziliezuliwa kutokana na mvua kubwa zilizoambatana na upepo mkali…
Na Katomali Nchimbi,Manyara-Babati
Mamlaka ya hali ya hewa Mkoa wa Manyara imeendelea kuwataka wananchi kuendelea kufuatilia Taarifa za utabiri wa hali ya hewa ili ziweze kuwasaidia katika kuendeleaza shughuli zao za kila siku pasipo kupata madhara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani Manyara.
Akizungumza kwenye kipindi cha Tubonge cha Smile fm Novemba 18,2026, Wilayani Babati Meneja wa mamlaka hiyo Mkoa wa Manyara Bi Salma Amour amesema kuwa wakati wa mvua hizi za vuli wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari pindi wanapoona mvua zinazoambatana na upepo mkali ili zisiweze kuleta majanga na amewataka wafugaji kuvuna maji ya mvua kwa njia za kisasa ili yawasaidie wakati wa kiangazi kipindi ambacho kunakuwa na ukame mkubwa na uhitaji wa maji kwa ajili ya mifugo yao.
sauti ya Salma Amour meneja TMA Manyara
Ameongeza kuwa kuna umuhimu wa mkulima na mfugaji kuwa karibu na wataalam wa kilimo na mifugo ili kupata taarifa za kitaalam ili mfugaji aepuke magonjwa yatokanayo na mvua na mkulima kuwa sambamba na afisa ugani apate usaidizi zaidi kwenye masuala ya kilimo kama aina gani ya mbegu zinapaswa kupandwa kwa wakati huu wa mvua kubwa.

Pichani ni bi Salma Amour na Haji Hamimu katika studio za Smile fm,(picha na Frank Kijukuu)
Kwa upande wake Muangazi wa Mamlaka ya hali ya hewa Mkoani Manyara Haji Hamimu amesema kwa Mkoa wa Manyara mvua hizo zilileta madhara kwa Wilaya ya Hanang kwenye kata ya Kateshi ambapo nyumba takribani 32 ziliezuliwa kutokana na mvua kubwa zilizoambatana na upepo mkali kunyesha kwenye Wilaya hiyo lakini hazikusababisha vifo kwa wakazi wa eneo hilo.
Ameongeza kuwa ni jukumu lao kama mamlaka kuujuza umma kuhusu masuala ya hali ya hewa,na amewataka wananchi kuacha kupuuza pindi zinapotolewa taarifa za utabili wa hali ya hewa itawasaidia kujikinga na kuchukua tahadhari mapema.
sauti ya Haji Hamimu muangazi TMA Manyara