Smile FM Radio

Nina la kujivunia kwenye Michezo…

11 October 2026, 5:16 pm

Pichani ni Mkurugenzi mkuu wa Fountaingate Academy and Sports, Japhet Mboto Makau akifuatilia jambo kwenye mahafari ya shule hiyo,(picha na Katomali Nchimbi)

Kwa kushirikiana na mkuu wa mkoa wa Arusha Amosi Makala aliamua kuipeleka timu ya fountagate fc, Arusha ili kuendelea kuleta hamasa ya jiji hilo.

Na Katomali Nchimbi.

Manyara-Babati

Mkurugenzi mkuu wa Fountaingate Tanzania Japhet Mboto Makau amesema anajivunia kuwa mmoja wa mdau mkubwa wa kulea,kukuza na kuibua vipaji vya vijana na watoto katika shule zake za Fountaingate academy and Sports.
Makau amezungumza hayo wakati wa sherehe za mahafari ya kuhitimu darasa la saba na pre unite yaliyofanyika Octoba 10,2026, Manyara katika viwanja vya shule hiyo vilivyopo eneo la mruki Babati mjini.

Sauti ya Japhet Makau Mkurugenzi mkuu wa fountaingate academy and Sports

Amesema kwa kushirikiana na mkuu wa mkoa wa Arusha Amosi Makala aliamua kuipeleka timu ya fountagate fc, Arusha ili kuendelea kuleta hamasa ya jiji hilo ukizingatia kwa wakati huo Arusha hapakuwa na timu ya ligi kuu hivyo Fountangate ndio ilikuwa timu ya kwanza ya ligi kuu bara kuhamia jijini Arusha.

Pichani ni baadhi ya wanafunzi wa fountaingate academy and sports waliohitimu darasa la saba 2026,(picha na Katomali Nchimbi)

Kwa upande wake Principal wa shule hiyo Joseph Msafiri Mjingo amesema wameanzisha chuo cha Michezo na wameanza kwa kozi ya riadha na mpira wa miguu pamoja na wakufunzi wa michezo mbalimbali ili kusogeza fursa kwa wahitaji na kuendelea kujitangaza ndani hadi nje ya mipaka ya Tanzania.

Pichani ni Joseph Msafiri Mjingo principal wa Fountaingate academy and Sports,(picha na Katomali Nchimbi.)

Sauti ya Joseph Mjingo principal foutaingate academy and sports

Ameongeza kuwa kumekuwa na maombi mengi kwa sasa kutoka kwa wadau na wapenzi wa soka mkoani Manyara kuomba timu hiyo irejee tena mkuoni humo, hivyo yeye na viongozi wengine wanatafakari kwa kina ili waone jinsi gani wanaweza kukubaliana ili waweze kuirudisha tena timu hiyo mkoani Manyara.

Pichani ni baadhi ya wazazi na walezi waliohudhuria mahafari hiyo,(picha na Katomali Nchimbi.)