Smile FM Radio

TAKUKURU manyara yabaini madudu

3 November 2026, 1:24 pm

Na Katomali Nchimbi,

Babati-Manyara,

TAKUKURU mkoani Manyara imetoa taarifa kwa umma kuhusu matukio mbalimbali utekelezaji na hatua zilizochukuliwa baada ya kugundua makosa katika miradi ya maendeleo na maeneo mengine.
Akizungumza na Waandishi wa habari kwenye ukumbi uliopo ofisi ya TAKUKURU Wilayani babati Mkoani Manyara Novemba 3,2026,naibu mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Antony Gang’olo,amesema kwa kipindi cha April hadi Septemba mwaka huu kupitia ofisi yake ya Wilaya ya Simanjiro imesaidia kurejesha kiasi cha sh.1,244,062 fedha za mradi wa ujenzi wa madarasa matatu na matundu ya vyoo sita katika shule ya msingi Namalulu.

Pichani ni naibu mkuu wa TAKUKURU mkoani manyara Antony Gang’olo akizungumza na waandishi wa habari,(picha na Katomali Nchimbi)

Baada ya ufuatiliaji kufanyika ilibainika kuwa marumaru box 26 zenye thamani ya sh.1,000.000 na Skirting box 6 zenye dhamani ya sh.244,062 hazionekani stoo japo kwenye nyaraka za manunuzi zinaonekana.
Ameongeza kuwa baada ya kubaini dosari mtendaji wa kijiji cha Namalulu ambaye ndiye msimamizi mkuu wa mradi akishirikiana na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Namalulu walidai kwamba vifaa hivyo vimeibiwa na waliomba kulipa fedha za vifaa hivyo.

sauti ya Anthony Gang’olo mkuu wa TAKUKURU manyara

Pichani ni baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kikao hicho,(picha na Katomali Nchimbi)

Aidha,wamefanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo 10 iliyopo Mkoani Manyara yenye thamani ya sh 2,831,279,108.75.