Smile FM Radio
Smile FM Radio
8 October 2026, 1:41 pm

Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara Martin Shigela akizungumza na Wafanyabiashara, (picha na Amedius Mushi.)
Baraza la Wafanyabiashara ni jukwaa muhimu linalowakutanisha wafanyabiashara wa sekta binafsi na serikali kwa lengo la kujadili na kutatua changamoto zinazoikabili.
Na Katomali Nchimbi
Manyara-Babati
Mkuu wa mkoa wa Manyara Martin Shigela amewataka wafanyabiashara kuchangamkia fulsa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana mkoani Manyara,akisisitiza kuwa Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano katika mchakato wote wa uwekezaji.
Shigela ameyasema hayo Octoba 6,2026,wakati akizungumza katika kikao cha wafanyabiashara Mkoa wa Manyara Wilayani Babati,ambapo ameeleza kuwa mkoa wa Manyara una fulsa nyingi katika sekta mbalimbali ukiachili mbali kilimo,uvuvi na ufugaji.
Ameongeza kuwa fursa hizo zinapaswa kutumiwa ipasavyo na wawekezaji kwa ajili ya kukuza biashara zao na kuchangia kuongeza ajira na kuleta maendeleo ya mkoa wa Manyara na Taifa kwa ujumla.

Pichani ni baadhi ya Wafanyabiashara waliohudhuria kikao na mkuu wa mkoa Manyara,(picha na Amedius Mushi)
Kwa upande wake afisa biashara mkoa wa Manyara,Ally Mokiwa amesema kuwa Baraza la Wafanyabiashara ni jukwaa muhimu linalowakutanisha wafanyabiashara wa sekta binafsi na serikali kwa lengo la kujadili na kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya biashara hapa nchini hasa mkoani Manyara.
Mokiwa amesema ushiriki huo unalenga kujenga Mazingira bora ya kufanya biashara na kuweka msingi wa dira ya maendeleo kuelekea mwaka 2050,na changamoto zinazowakabili Wafanyabiashara zitaendelea kushughulikiwa kupitia majadiliano ya pamoja kati ya serikali na sekta binafsi.

Pichani ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mati Super Brand LTD,David Mulukozi akichangia hoja kwenye kikao na mkuu wa mkoa,(picha na Amedius Mushi)
Aidha,Mkurugenzi wa Mati Super Brand LTD,David Mulukozi amesema Wafanyabiashara wanatarajia mawazo na fulsa za kibashara wanazowasilisha kupitia kituo hicha cha PPP kupewa kipaumbele.
Mulukozi ameongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kuwapa wawekezaji wa ndani nafasi zaidi ya kushiriki katika fulsa za zabuni na miradi mbalimbali pale zinapotangazwa.