Smile FM Radio

TPDC yatoa mafunzo kwa vyombo vya Habari

14 September 2026, 12:36 pm

Picha ya Katibu Tawala Msaidizi anayesimamia Sekta ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Manyara, Faraja Ngerageza

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limekutana na waandishi wa habari Mkoa wa Manyara katika mafunzo ya siku moja yaliyofanyika mjini Babati, Septemba 10, 2026, kwa lengo la kutoa elimu kuhusu shughuli za mafuta na gesi nchini.

Na Katomali Nchimbi

Akizungumza na waandishi wa habari katika mafunzo hayo, Katibu Tawala Msaidizi anayesimamia Sekta ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Manyara, Faraja Ngerageza amesema maeneo ambayo bomba hilo limepita wananchi wataimarika kiuchumi kutokana na baadhi yao watapata ajira mbalimbali ukiachilia mbali fidia zitakazolipwa wakati wa shughuli za ujenzi wa bomba hilo.

Ngerageza  Ameongeza kuwa kwa Mkoa wa Manyara bomba hilo limepita kwenye wilaya mbili  ambazo ni Kiteto na Hanang takribani watu 494  waliathiriwa na mradi huo huku watu 491 wamelipwa fidia zao kutokana na mradi huo katika Wilaya hizo za Mkoa wa Manyara.