Smile FM Radio
Smile FM Radio
15 September 2026, 3:21 pm

Picha ya Studio ya Smile Fm imepigwa na Katomali Nchimbi
Wazazi na Walezi kuwapatia Lishe bora ili kuwalinda na Magonjwa Nyemelezi ya Kudumaza Afya zao kwa kukosa lishe bora,na kutunza Mazingira ikiwemo kusafisha Vichaka na kuchoma moto, kuyaweka Mazingira Safi na Salama.
Na Katomali Nchimbi
Afisa ustawi wa Jamii Mkoa wa Manyara Bi Khadija Muhongo amewaasa Wananchi wa Mkoa wa Manyara kuendelea kuwa karibu na Familia zao ili kuepusha Madhara yanayoendelea kutokea kwenye kaya zao hasa watoto kupotea kwa kukosa uangalizi mzuri.
Akizungumza na Smile fm Radio Wilayani Babati, kwa njia ya simu Septemba 13/2026 Muhongo amefafanua jinsi gani Familia zinapaswa kuwa karibu na Jamii zao ili kuwalinda na Matukio ya Kikatili dhidi ya Watoto yanayojitokeza kwenye Maisha ya kila siku.
Amezungumzia pia suala la Malezi bora kwa Watoto na kuwakumbusha Wazazi na Walezi kuwapatia Lishe bora ili kuwalinda na Magonjwa Nyemelezi ya Kudumaza Afya zao kwa kukosa lishe bora,na kutunza Mazingira ikiwemo kusafisha Vichaka na kuchoma moto, kuyaweka Mazingira Safi na Salama.
Sauti ya Khadija Muhongo Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Manyara