Smile FM Radio

Bodaboda wasakwa Manyara

9 October 2026, 5:16 pm

Pichani ni Mrakibu wa polisi Mkoa wa Manyara Michael Mwakasungura RTO na Johnson Philipo mkaguzi wa Magari,mtahini wa Madereva,(picha na Frank Kijukuu)

Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani Mkoani Manyara limeanzisha msako makali juu ya wale wanaovunja sheria za barabara.

Na Katomali Nchimbi

Manyara-Babati

Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara kitengo cha usalama barabarani kupitia kwa Mrakibu wa jeshi hilo Michael Uswege Mwakasungura limewataka Maafisa usafirishaji maarufu bodaboda kufuata sheria za barabara ili kuepuka ajali zinazojitokeza mara kwa mara.
Akizungumza na Smile fm redio katika kipindi cha Tubonge Octoba 8,2026,Wilayani Babati Mkoani Manyara,Mwakasungura amesema kuwa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kazi yao ni kusimamia sheria kwa mtumiaji wa barabara na kushughulika na wanaozivunja sheria hizo.

Sauti ya Michael Mwakasungura Mrakibu wa jeshi la polisi mkoani Manyara

Ameongeza kuwa Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani Mkoani Manyara limeanzisha msako makali juu ya wale wanaovunja sheria za barabara ikiwemo kuzikata pikipiki na kubadirisha taa, wasiovaa kofia ngumu wanapoendesha pikipiki pamoja na wasiokuwa na vigezo vya kisheria vinavyowapa ruksa ya kuendesha vyombo vya moto.

Pichani ni Michael Mwakasungura R.T.O mkoa wa Manyara,(picha na frank Kijukuu)

Kwa upande wake Sajenti wa polisi Johnson John Philipo Mkaguzi wa Magari na Mtahini wa Madereva,amewata madereva kurudi shule ili kuongeza ujuzi kwani sheria zinaongezeka kila siku hivyo kuna umuhimu kwao kuendelea kusoma ili kuzifahamu sheria kwani uzoefu pekee hautoshi.
Mwakasungura ametoa rai kwa maafisa usafirishaji kuacha kutumika kwenye uhalifu kwasababu yapo mashtaka yanayohusiana na baadhi yao pikipiki zao kutumika iwe kwa kujua au pasipokujua kufanya uhalifu.

Sauti ya mkaguzi wa magari na mtahini wa madereva wa jeshi la polisi Johnson John Phillipo