Smile FM Radio
Smile FM Radio
19 September 2026, 4:24 pm

Picha ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara Martin Shigela,imepigwa na Katomali Nchimbi
Kuanza kuchukua Tahadhari Mapema ili kuepuka Madhara
Na Katomali Nchimbi
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Martine Shigela, ameongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kutembelea na kukagua maeneo mbalimbali yanayoweza kuathiriwa na mvua za El-Nino zinazotarajiwa kunyesha katika maeneo mbalimbali Nchini kuanzia mwishoni mwa mwezi Septemba na mwanzoni mwa Octoba 2026.
Wakizungumza mbele ya Mkuu wa mkoa wa Manyara Septemba 18/2026,katika Kijiji cha Maole, Diwani wa Kata ya Magara Timoth Gonzala na Mwananchi wa Kata hiyo Elizabeth Francis wamemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa kuna mvutano wa maouni kwa baadhi ya Maeneo na kuonyesha Hofu yao endapo Mvua hizo zikianza kunyesha na kusababisha Madhara makubwa kwa Wakazi wanaofanya Shughuli zao za kila Siku pembezoni mwa Mlima Magara.
Shigela ametoa maelekezo kwa Kamati hiyo ya ulinzi na usalama ya Mkoa kuanza kuchukua tahadhari Mapema ili kuepuka Madhara na ameupongeza uongozi wa Kijiji kwa kujitolea kutoa Mafuta pindi Mtambo wa kutanua Mto huo utakapofika Kijijini hapo.
Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Martin Shigela