Micheweni FM

‘Ulemavu isiwe sababu ya kutoshirikishwa katika michezo mashuleni’

25 November 2024, 12:43 pm

Wanafunzi wa skuli ya Minungwini Msingi wakiwa wametoka madarasani kwa ajili ya kipindi cha michezo

Ulemavu ni hali ya kuwa na hitilafu ya kudumu mwilini au akilini inayomzuia mtu kutekeleza shughuli zilizo kawaida katika maisha ya jamii. Unamwekea mtu mipaka asiweze kutekeleza shughuli fulani katika maisha yake, tofauti na watu wengine.

Na Mwiaba Kombo

Nchini Tanzania katiba ya 1977 ilitambua haki za watu wenye ulemavu na kukataza aina zote za ubaguzi. Mnamo mwaka wa 2004, Wizara ya kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo ilitoa Sera ya Taifa ya watu wenye ulemavu, inayosisitiza kujitolea kwa wizara hiyo katika kuhakikisha kwamba kuna haki sawa kwa watu wenye ulemavu.

leo tutazungumzia ushiriki wa wanafunzi wenye ulemavu kwenye michezo maskulini ambapo Makala hii inaletwa kwako na Mwiaba Kombo Hamad, kwa ushirikiano wa Chama Cha Waandishi Wa Habari Wanawake, Tanzania, Zanzibar (TAMWA Zanzibar) kupitia mradi wa Michezo kwa Maendeleo unaotekelezwa   chini ya ufadhili Taasisi ya Maendeleo ya Mashirikiano ya Ujerumani (GIZ)  nikusihi tuwe pamoja mwanzo hadi mwisho wa Makala hii .