Wafanyabiashara soko la Konde Pemba walilia wateja
6 November 2024, 12:50 pm
Soko la Konde ambalo lipo wilaya ya Micheweni ni miongoni mwa masoko ya kisasa ambayo yalijengwa kwa lengo la kuhakikisha wafanya biashara wadogo wadogo wanakwenda sokoni hapo kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za biashara .
Na Mwiaba Kombo
Wafanyabiashara wa soko la Konde wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wametakiwa kudumisha usafi katika soko hilo ili kujiepusha na maradhi ya mlipuko katika eneo lao.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira na Afya ya halmashaauri ya wilaya ya Micheweni katika ziara ya kutembelea soko hilo pamoja na makazi ya wanajamii kwa lengo la kuangalia usafi katika maeneo hayo.
Aidha mwenyekiti huyo amewataka wafanya biashara hao kutokuuza biashara zao nje ya soko badala yake waingia ndani ya soko kwani ni sehemu salama zaid kwao.
Kwa upande wake katibu wa kamati hiyo ambae pia ni afisa afya na mazingira wa halmashauri hiyo Rashid Abdalla Seif amesema ni kuangalia hali halisi katika soko na konde pamoja kuangalia wauzaji wa bidhaa mbali mbali katika soko hilo ikiwemo mboga mboga ,samaki ,nyama pamoja na bidhaa nyengine.
Amesema usafi ni jambo muhimu katika jamii hivo vyema mfanya biashara na mwanajamii anaweka usafi katika mazingira yake anayofanyia kazi pamoja na anayoishi .
Nao wafanya biashara katika soko hilo wamesema bado kuna changamoto ya uzaji wa biasha katika soko hilo na wameiomba serikali kupitia halmashauri kupunguziwa ushuru pamoja na kufanyanyika ukarabati kwa baadhi ya maeneo katika soko hilo.