Koica yawapiga msasa wakaguzi wa walimu Pemba
29 October 2024, 3:50 pm
Mkaguzi mkuu wa elimu Zanzibar Maimuna Fadhil Abas akizungumza na wakaguzi wa walimu wakati wa ufunguzi wa mafunzo huko kituo cha walimu (TC)Michakaeni chake chake Pemba (picha na Mwiaba Kombo)
Taasisi ya kuboresha elimu Zanzibar lengo lake kubwa ni kuhakikisha wakaguzi pamoja na walimu wa Zanzibar wanapata mafunzo ambayo yatawawezesha katika kufanya kazi zao kwa ustadi mkubwa na wenye tija kwa wanafunzi.
Na Mwiaba Kombo
Wakaguzi wa walimu kisiwani Pemba wametakiwa kuwasaidia walimu ili kuweza kufikia malengo ya elimu yaliyokusudiwa .
Wito huo umetolewa mkaguzi mkuu wa elimu Zanzibar Maimuna Fadhil Abas wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya wakaguzi katika kituo cha walimu Michakaeni chake chake Pemba.
Amesema endapo walimu hawatawezeshwa katika kupatiwa mafunzo na sapoti kutoka kwa wakaguzi hakuna kitu hata kimoja ambacho kitakwenda sawa .
Maimuna amewataka wakaguzi hao kuhakikisha wanayafanyia kazi mafunzo wanayopatiwa ili iweze kusaidia walimu maskulini .
Kwa upande wake meneja wa mradi wa kuboresha elimu Zanzibar (GOOD NEIGHBORS)Ye Cheng amesema lengo la mradi huo ni kuongeza ubora maskulini na kuhakikisha walimu na viongozi wa maskulini wanafanya kazi kwa mashirikiano kwani ndio msingi wa mafanikio .
Amesema kuna mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu ambayo ymaepatikana baada ya kuja mradi huo.
Nae mratibu wa wakaguzi Pemba Dr. Amour Rashid Ali amemuhakikishia meneja mradi huo kufanya kazi kwa mashirikiano kwani ni sehemu ya utekelezaji wa kuwawezesha wafanya kazi kufanya kazi kwa ufanisi .
Nao mwenyekiti wa wakufunzi Simon Gerald Shayo pamoja afisa mradi mkuu ABERHARD PHINIAS wamesema ushirikiano baina ya wakaguzi na walimu wakuu na walimu wengine ndio kitu kinachohitajika katika uendaji wa kazi.
Mafunzo hayo ya siku nne yameanza leo octber 29 na yanatarajiwa kumalizika siku ya Ijuma ya Nov 1 ambapo wakaguzi wa skuli za maandalizi ,msingi na sekondari kisiwani Pemba wameshiriki katika mafunzo hayo.