Uvinza FM

Mazoezi ni muhimu kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza

24 December 2025, 7:19 pm

Wafanyakazi wa hospitali ya kabanga wakifanya mazoezi ya pamoja na wananchi katika wiki ya afya kabanga. picha na Emmanuel Kamangu

Tunatakiwa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo pia kuendelea kujenga afya zetu.

Na Emmanuel Kamangu.

Wananchi wilayani kasulu wametakiwa kujenga tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kujenga afya zao.

Ushauri huo umetolewa na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa Kabanga, Dkt. Peter Kitenyi wakati wa kuhitimisha  zoezi maalumu la utoaji wa huduma ya vipimo bure  ikiwa ni wiki ya fya kabanga ambapo amewasihi wananchi waliojitokeza kufanya vipimo mbali mbali  kuzingatia mazoezi  ili kuwa na afya tele.

Wakati huo huo  Dkt. Kitenyi amesema zaidi ya wananchi 700 wamepata huduma za vipimo bure katika wiki hii  ya afya kabanga  jambo ambalo ametaka ni mwanzo mzuri katika kuiweka jamii karibu na hospitali hiyo.

Mmoja wa watumishi wa hospital ya kabanga  Bi, Flora Ntahondi akizungumza kwa niaba ya watumishi wenzake amesema kusudio kubwa  la kutoa huduma ya vipimo bure kwa wananchi ni kuwasaidia kuwajengea uelewa juu ya kutambua umhimu wa  kupima  afya zao mara kwa mara.

Zoezi hili la kampeni ya wiki ya afya kabanga hufanyika kila mwaka lengo ikiwani  kutoa hamasa kwa nananchi kuelewa umhimu wa mazoezi na kutambua umhimu wa kujua afya zao kwa kufanya vipimo kila wakati.