Uvinza FM
Uvinza FM
15 May 2025, 8:31 pm

Vikundi vya wajasiriamali wa halamashauri ya wilaya ya Uvinza waanza kunufaika na elimu iliyoanza kutolewa hii leo mei 15 juu ya mkopo wa asilimia kumi wa mama Samia.
Na Linda Dismas
Vikundi vya ujasiriamali katika wilaya ya Uvinza leo Mei 15, 2025 wameanza mafunzo ya ujasiriamali yatakao chukua muda wa siku sita, kwa lengo la kupewa elimu kabla ya kupatiwa fedha ya mikopo ya asilimia 10 itakayo wasaidia kujikwamua kiuchumi.

Picha ya maafisa maendeleo ya jamii wilaya ya uvinza, kulia ni Bi. Leah Stanilei Mjema.
Akizungumza na uvinza fm redio Bi.Leah Stanilei Mjema ambaye ni afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Uvinza amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha mwanakikundi anakuwa na uelewa mkubwa wa namna ya kukuza biashara zao mara tuu wanapopata mkopo.
Aidha amewataka akina baba kuonyesha ushirikiano wao kwa kina mama waliochukua mkopo wa asilimia 10 ili kufikia malengo yao ya kujikwamua kiuchumi.
Vilele Bi.Leah amewashauri wananchi kutumia fursa hiyo ya mkopo wa Mama Samia ili kuendeleza shughuli zao za kibiashara na ujasiriamali.

Naye mtendaji wa kata ya Uvinza Bw.Edward Amos amesema ni vyema kila mwanakikundi kutambua katiba ya kikundi inasemaje ili kuepusha migogoro.
Akijibu swali liloulizwa na mmoja wa wanavikundi hivyo vya ujasiriamali “ni kwanini baadhi ya fomu za mikopo zinaenda kwenye kikundi zikiwa na muhuri wa mtendaji ila jina sio lake” ambapo mtendaji amejibu kuwa kila mtu atambue kuwa cheo sio mtu wala jina la mtu.
Nae Fadhila Sadick mmoja wa kikundi cha RAHA DELICIOUS ametoa shukrani zake kwa viongozi wa maendeleo ya jamii kwa kuwapa elimu ya namna ya kuendesha biashara pale tuu watakapopata mikopo ili iweze kuwasaidia kukuza biashara zao.