Uvinza FM
Uvinza FM
12 May 2025, 2:36 pm

Toka kuundwe kwa dawati la kijinsia katika shule hiyo wanafunzi wamepata elimu ya kufahamu madhara ya mimba za utotoni na kufahamu namna ya kuepuka vishawishi
Na Theresia Damasi
Katika kuhakikisha ukatili dhidi ya watoto unakomeshwa na kupingwa vikali katika jamii,Shule ya msingi muungano katika halmashauri ya wilaya uvinza imeeunda dawati la ukatili kwa ajili ya kuwapa watoto elimu ya njinsi ya kukabiliana nao.
Wakizungumza na uvinza fm redio katika kipindi cha school Baraza wanafunzi wa darasa la sita na la saba wamesema toka kuundwe kwa dawati la kijinsia katika shule hiyo wamepata elimu ya kufahamu madhara ya mimba za utotoni na kufahamu namna ya kuepuka vishawishi.
Katika kupanua mjadala wa mada ya madhara ya mimba za utotoni wanafunzi hao wameeleza ni wapi wanapaswa kutoa taarifa wanapofanyiwa ukatili.

Naye mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi muungano Paulo Mandai ameeleza umuhimu wa dawati la jinsia katika shule hiyo ambapo amesema wazazi wawape watoto elimu ya kijinsia bila kupepesa macho.
Hata hivyo mwalimu Mandai ameeleza chanzo cha mimba za utotoni huku akiwataka wazazi wawe walimu wa kwanza kuwafundisha watoto maadili mema na kupinga ukatili unaofanywa dhidi ya watoto.