Uvinza FM

Kamati ya afya msingi Uvinza kutoa elimu ya magojwa ya mlipuko

29 March 2025, 7:09 pm

Mratibu wa malaria wilaya ya Uvinza na washiriki katika mafuzo ya magonjwa ya mlipuko na malaria. picha na Abdunuru Shafii

Kila mmoja anatakiwa kutimiza wajibu wake kwa kuchukua tahadhari kwa kila hatua ili kujikinga na kuwakinga wengine.

Na Abdunuru Shafii

Kamati ya afya ya msingi ya wilaya ya Uvinza imefanya kikao katika ukumbi wa halmashauri kwa lengo la kutoa elimu juu ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu, M-Pox na ugonjwa wa malaria huku washiriki wakiwa wananchi, waganga wa tiba asili, viongozi wa dini na viongozi mbalimbali wa serikali.

Mgeni rasmi katika kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi. Dinnah Mathamani amewataka kila mmoja kutimiza wajibu wake kwa kuchukua tahadhari kwa kila hatua ili kujikinga na kuwakinga wengine kutokana na magonjwa ya mlipuko.

Sauti ya mkuu wa Wilaya Uvinza

Mratibu wa Ufuatiliaji wa Magonjwa ya Mlipuko (IDSR), Charles Mbise, ameeleza dalili na jinsi ugonjwa wa M-Pox unavyoambukizwa kutoka kwa wanyamapori kwenda kwa binadamu  na kutoka kwa binadamu kwenda kwa binadamu mwingine.

Sauti ya Mratibu wa Ufuatiliaji wa Magonjwa ya Mlipuko (IDSR) Charles Mbise

Nao viongozi wa dini wameeleza namna ambavyo wamekuwa wakitoa elimu kwa jamii, ambapo wamesema wameweka mikakati ambayo wataendelea kuitumia kuhakikisha elimu hii inaendelea kuwafikia wananchi wanaowahudumia.

Sauti za viongozi wa dini