Suluhisho la Vifo vya Wajawazito lapatikana
21/04/2021, 10:22 am
KIGOMA
Na, Glory Paschal
Serikali ya Mkoa wa Kigoma ikishirikiana na wadau wa Afya imezindua mpango wa dharula wa miaka mitatu ya kukabiliana na vifo vya mama mjamzito na mtoto mchanga ambavyo kwa sasa vimeongezeka na kufikia asilimia 95 katika vituo vya afya
Kwa mujibu wa takwimu za afya mkoani hapa ongezeko hilo limeelezwa kuchangiwa na idadi ndogo ya wahudumu wa afya wenye uwezo mdogo katika vituo vya kutolea huduma sanjari na miundombinu rafiki ya kumuwezesha mama mjamzito kufika kituoni mapema wakati wa kijifungua
Kwasasa wahudumu wa afya mkoani Kigoma ni asilimia 33 hali inayopelekea utoaji wa huduma kuwa ni changamoto na kusababisha kila baada ya siku tatu mwanamke mmoja kupoteza maisha kwasababu ya uzazi huku kila siku watoto wachanga watatu hupoteza maisha
Aidha baadhi ya mashirika yakiwemo UNICEF, WHO,UNFPA Kigoma Joint program yametoa msaada wa vifa vya dharula ili kuwezesha wajawazito kujifungulia katika vituo vya afya kwa wakati
Kwa upande wake MKuu wa mkoa wa Kigoma kamishna wa Polisi Thobias Andengenye alikuwa na haya ya kuzungumza Juu ya Mpango wa dharula wakukabiliana na vifo kwa mama mjazito na mtoto mchanga
Mpango wa dharula wa kukabiliana na vifo vya mama mjazito na mtoto mchanga Mkoani Kigoma unalenga Kupunguza vifo vitokanavyo na Uzazi, ongezeko la wanawake wajawazito kufika Kliniki, kupunguza vifo kwa watoto wachanga, Kuongeza idadi ya watoa huduma ngazi ya jamii na Kuongeza matumizi ya njia za Uzazi wa Mpango.