Mnara umerejea ni 3G tena
13 December 2024, 5:40 pm
Na Joel Headman Babati
Ndio..baada ya msoto wa karibu miezi miwili kwenye uwanja wa nyumbani bila ushindi wa ligi, hatimaye Fountain Gate wamepata alama 3 leo dhidi ya Coastal Union ya Tanga yenye makazi ya muda Jijini Arusha.
Mara ya mwisho Fountain Gate kupata ushindi wa ligi kuu kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa Babati ilikuwa 21 Oktoba 2024 walipoilaza KMC kwa mabao 3-1 Toka hapo imeshinda mchezo mmoja tu wa Shirikisho dhidi ya Mweta SC ya mwanza Jumamosi iliyopita kwa ushindi wa 2-0.
Mchezo wa leo uliopigwa saa 8 mchana umekuwa mkali na wa kuvutia kutokana na mbinu za waalimu Mohamed Muya wa Fountain na Juma Mwambusi wa Coastal kuonyesha uwezo wa kushambuliana kwa vipindi.
Licha ya Coastal kuongeza makali dakika za mwishoni walifaidika tu kupata goli la pili ambalo limedumu mpaka mwisho wa Mchezo.
Akizungumza na Triple A fm mwalimu wa Fountain Mohamed Muya amesema ushindi huu unawapa nguvu kubwa ya kuendelea kupambania alama 3 hasa katika mchezo ujao wa ugenini dhidi ya Azam.
Kwa upande wake kocha wa Coastal Union Juma Mwambusi amelaumu uzembe wa wachezaji wake na kueleza umesababisha kufungwa goli 3.
Mechi zijazo kwa timu zote 2 zitakua ugenini ambapo Fountain Gate wataelekea Chamazi kuumana na Azam wakati Coastal wakiwafuata wababe wa Yanga Tabora United