Triple A FM

Coastal, Prisons mpaka baadaye

1 December 2024, 5:23 pm

Muonekano wa uwanja wa Sheikh Amri Abeid baada ya mvua kunyesha

Na Joel Headman Arusha

Unazijua sababu zinazoweza kusababisha mchezo kuahirishwa?

Mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara kati ya Coastal Union na Tanzania Prisons umepigwa kalenda.

Mchezo huo namba 102 uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha umeshindikana kutokana na mvua inayoendelea kunyesha Jijini Arusha.

Timu zote mbili zilikamilisha ratiba ya kufanya mazoezi mepesi ya kupasha misuli joto kuonyesha zipo tayari kwa mchezo lakini kwa bahati mbaya zilipoingia vyumbani kubadili jezi na kuanza kucheza hazikutoka tena sababu ya mvua.

Kwa mujibu wa kanuni za bodi ya ligi kuu miongoni mwa sababu za kuahirishwa kwa mchezo ni pamoja na uwanja kuwa kwenywe hali ya kutoruhusu mpira kudunda.

Sababu hiyo imetosha kusogeza mbele mchezo huu mpaka hapo taarifa zaidi itakapotolewa na bodi ya ligi kuu.

Hata hivyo kanuni zinaelekeza kuwa iwapo mchezo utaahirishwa kwa sababu tajwa hapo juu unapaswa kurudiwa saa 4 asubuhi ya siku inayofuata kumalizia dakika zilizosalia au kama haukuchezwa kabisa uanze upya.