Triple A FM

Kengold hali tete inapumulia mashine

12 September 2024, 1:45 pm

Mchezaji Kasim Hamis wa Fountain Gate akishangilia baada ya kuisawazishia timu yake

Joel Headman Babati

Timu ya mpira wa miguu ya Kengold kutoka Mbeya imeendelea kupumulia mashine kwenye ligi kuu Tanzania bara baada ya kukubali kipigo kingine toka kwa Fountain Gate fc ya Manyara.

Katika mchezo huo namba 18 mzunguko wa 2 uliopigwa Sept 11 kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa ulioko Babati Mkoani Manyara Kengold ndio waliotangulia kufunga goli dakika ya 9 kabla ya kibao kugeuka na kuanza kuteseka dakika ya 42 Fountain Gate waliposawazisha na kupata goli lingine dakika ya 58 lililoizamisha kabisa Kengold kwa matokeo ya 2-1.

Huu unakua mchezo wa 2 mfululizo ikipoteza hali inayoweza kuweka shakani kibarua cha kocha wake Fikirini Elias ambaye mwishoni mwa wiki hii atakuwa na kibarua kizito ugenini mbele ya Kino boys KMC kwenye uwanja wao jijini Dar Es Salaam.

Kocha wa Kengold

Hata hivyo kocha huyo amesema hana wasiwasi kwani anaendelea kuwanoa vijana wake na ana imani watabadilika.

Kwa upande wake kocha wa Fountain Gate fc Mohamed Muyo ameomba mashabiki wa timu hio kuendelea kujitokeza viwanjani kwa wingi ili kuifanya timu yao ipate ushindi zaidi.

Kocha wa Fountain Gate

Mchezo huu umekuwa wa kihistoria kuchezwa hapa Babati kwani mkoa huu wa Manyara haujawahi kuwa na timu ya ligi kuu toka nchi ilipopata uhuru mwaka 1964. Wakazi wa Babati wataendelea ku enjoy burudani ya ligi kuu leo majira ya saa 10 kwenye mchezo mwingine utakaozikutanisha Dodoma jiji na Namungo