Adhana FM

Kukosekana hati miliki chanzo cha migogoro ya ardhi CP HAMAD

13 June 2024, 4:23 pm

Na Said Bakar, Zanzibar

Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad amesemaa kesi nyingi za migogoro ya ardhi zinazoripotiwa vituo vya Polisi chanzo chake ni kukosekana kwa hati miliki za maeneo hayo.

Ameyasema hayo huko Makao Makuu ya Polisi Zanzibar alipokua akikabidhiwa hati ya umiliki ardhi katika maeneo ya Polisi Mazizini, Bumbwini na Mkokotoni amesema kukabidhiwa kwa hati hizo kutapelekea kuepusha migogoro na kuendelezwa kwa maeneo hayo.

Aidha amewaagiza Makamanda wa Polisi wa Mikoa yote ya Zanzibar kuhakikisha wanakagua maeneo yote ya Polisi na kuhakikisha yanapatiwa hati miliki.

Akikabidhi Hati hizo Mkuu wa kitengo cha Hati kutoka Kamisheni ya Ardhi Eng. Ali Kessi Ali amesema umiliki wa hati unapelekea maeneo kua salama na kuepuka kuvamiwa na watu wengine.