Jumuiya ya Istiqama Zanzibar, yatoa semina elekezi kwa mahujaji huko Makka
12 June 2024, 7:34 pm
Na Mwandishi Wetu, Makka Saud Arabia.
Mahujaji waliosafiri na Jumuiya ya Istiqama Zanzibar, wamepewa semina elekezi kabla ya kuaza kwa ibada ya hija huko Makka Saudi Arabia.
Semina hiyo kwa upande wa wanaume imeongozwa na Sheikh Suweid Ali Suweid katika kuwafundisha mambo muhimu ya ibada, mahujaji namna ambavyo watatekeleza nguzo hiyo ta tano ya uislamu ambayo itakayoanza mwezi 8 Dhulhijja 1445 Hijiria, inayojuulikana kama siku ya Tarwiya, ambapo mahujaji watalazimika kutia nia ya kuhirimia, na kuvaa nguzo za ihraam.
Aidha kwa upande wa wanawake, semina hiyo imeongozwa na Sheikh Rashid Al Rasady ambaye amewafunza mambo yote yanayonasiniana na ibada ya hijja.
(Baadhi ya Mahujaji waliosafiri na Jumuiya ya Istiqama Zanzibar wakifuatilia semina elekezi kabla ya Ibada ya Hijja huko Makka-Saud Arabia)
Sheikh Suweid amesema kuwa siku hiyo mahujaji wataaelekea mji wa Minna na baada ya hapo, siku ya mwezi tisa (9) Dhulhijja mahujaji wataelekea viwanja vya Arafa baada ya kuchomoza kwa jua, na watakaa hapo mpaka jua litapozama na baada ya hapo, mahujaji watalala Muzdalifa.
Ama baada ya kusimama Arafa, mahujaji hao, wataelekea Mina na kupiga mawe katika jamrat ambapo siku ya mwezi 10, Dhulhijja, wataelekea Masjid haraam kufanya twawaaf na sai, baada ya kuchinja na kunyoa, ikisha watarudi tena Mina kwa kulala na kumaliza kupiga mawe katika jamrat zilizo bakia. .
Ama kwa wale ambao hawatoweza kutufu siku ya 10, watatufu na kufanya sai, ambao watarusha vijiwe na kurudi Minna na mwezi 12 watamalizia twawaaf na sai, na itakuwa wamekamilisha ibada yao ya hijja.