Adhana FM

Makamu wa Pili wa Rais, awahimiza Watu Wenye Ulemavu Kuchangamkia Fursa za Maendeleo Nchini

2 June 2024, 9:34 pm

Na Nishan Khamis, Kaskazin Unguja

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewahimiza watu wenye ulemavu kuchangamkia na kuzifikia fursa za kimaendeleo nchini kwani wana haki kuzifikia fursa hizo kwa misingi ya kujiinua kiuchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Mhe. Hemed ameeleza hayo leo katika kiwanja cha mpira Mto wa Pwani wilaya ya kaskazin A Unguja wakati akizungumza na viongozi, wananchi na wanachama wa jumuiya ya wasioona Zanzibar kwa niaba ya Rais wa Zanzibar, Dkt Husein Ali Mwinyi wakati wa kuahirisha maadhimisho ya kuongeza uwelewa kwa jamii juu ya watu wenye ulemavu mkoa wa kaskazini Unguja.

Makamu wa pili wa Rais, amesema serikali ya mapinduzi ya zanzibar inatambua na kuthamini mchango mkuwa wa maendeleo yanao tokana na watu wenye ulemavu nchni, hivyo kutokana na mchango wao serikali imejenga skuli jumuishi, masoko, utoaji wa mikopa na uwepo wa mfuko wa maendeleo wa watu wenye ulemavu ni utekelezaji wa ilani CCM kwa watu wenye uleamavu nchini.

Halikadhalika Hemed amesisitiza suala la kuhamasisha watu wenye mahitaji maalumu kuzikimbilia fursa pamoja na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu kwa kuweka misingi imara ya maendeleo nchini.

Akizungumza katka maadhimisho hayo mkuu wa mkoa wa kaskazini Unguja Rashid Hadid Rashid, amesema katika kutambua na kuthamini michango yao, serikali imeandaa mipango madhubuti ya kuwasaidia na kuwainua kiuchumi pamoja na kutatua changamoto mbali mbali zinazo wakabili Aidha RC Hadid amewasihi kuwa na subra katika kipindi hichi kifupi pindi mchakato utakapo kamilika basi wafuate taratibu za kisheria katika upatikanaji wa mikopo kwa misingi ya maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla.

Awali akisoma risala katika hafla hiyo Awena Hassan Seif kutoka jumuiya ya watu wenye ulemavu, alieleza kuwa jumuiya hiyo imempongeza Rais Dkt Husein Mwinyi kwa jitihada kubwa alizofanya za kimaendeleo katika mkoa huo katika kipindi miaka 3 ya uongozi wake.

Awena ameeleza kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Ulemavu si kikwazo cha kufikia maendeleo ” hivyo ameiomba serikali kufanyia haraka kukamilika mchakato wa sheria na sera za watu wenye ulemavu pamoja na kupatiwa hati miliki ya kituo cha watu wasioona kilichopo Chaani Lunga Lunga.