Mbunge wa Chaani Juma Usonge akabidhi vifaa vya ujenzi skuli ya msingi Kikobweni
2 June 2024, 3:05 pm
Na Juma Haji, Adhana FM.
Mbunge wa jimbo la Chaani Juma Usonge amekabidhi vifaa vya ujenzi, vikiwemo matofali, mchanga, saruji, mawe, na nondo kwa ajili ya ujenzi wamadarasa matatu ya skuli ya misingi Chaani kikobweni .
Amesema kuwa, miongoni mwa vifaa vilivyotolewa ni matofali 2800, tani 24 za mchanga, saruji mifuko 98, mawe gari 8 na nondo 38 kwa ajili ya ujenzi madarasa matatu ya skuli ya misingi Chaani kikobweni.
Mbunge huyo ameeleza kuwa huo ni muendelezo wake katika kutatua changamoto za ukosefu wa madarasa kwa wanafunzi katika jimbo lake kwani katika kipindi cha miaka 4 tayari amejenga skuli tatu na anaendelea na kazi hiyo katika kuimarisha misingi mizuri ya kielimu na kiafya katika jimbo hilo.
Usonge amewahakikishia wanachi kuwa ataendelea kushirikiananao kwa hali na mali pamoja na kuunga mkono juhudi za maendeleo katika miradi iliyopo katika jimbo hilo
Afisa elimu mkoa wa kaskazini Unguja Subira Abdalla Vuai, ameeleza kuwa bado kuna changamoto ya uhaba madarasa kwenye skuli za Mkoa huo, hivyo kitendo cha mbunge kuendeleza jitihada za ujenzi wa madarasa, kutasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto hiyo katika jimbo hilo .
Nao wananchi wamesema wanaendelea kuunga mkono juhudi za mbunge wao kwani amekuwa karibu na jamii kwa hali zote na husuaan kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo mwendelezo wa ujenzi wa vyumba vya madarasa vya skuli na vituo vya afya katika jimbo hilo
(Habari hii imeandikwa na Juma Haji na kuhaririwa na Ali, Khamis M)