Watu wenye ulemavu na mahitaji maalumu wasifichwe majunbani-DC Kaskazini “A”
2 June 2024, 1:27 pm
Na Nishan Khamis, Kaskazin Unguja .
Mkuu wa wilaya ya kaskazini “A” Unguja Othman Ali Maulid amesema kuwa kuwafungia ndani watu wenye ulemavu na mahitaji maalumuni kosa kisheri na kuwakosesha haki zao za kimsingi katika nyanza zote.
DC Othman ameyasema hayo katika ufunguzi wa kongamano la watu wenye mahitaji maalum mkoa wa kaskazini Unguja, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano chuo cha Mafunzo ya amali huko Mkokotoni, shughuli imeandaliwa na jumuiya ya watu wsioona mkoa wa kaskazini Unguja.
Amekumbusha masheha kufanya ufuatiliaji wa watu wenye mahitaji maalumu pamoja na kuwahamasisha kuchangamkia fursa za maendeleo zilizopo katika jamiii.
Akizungumza katika Hafla hiyo Mwenyekiti wa jumuiya wasio ona Zanzibar Bi Fatma Djaa Chesa amesema lengo la mkutano huo ni kuifahamisha jamiii kuwa, watu wenye ulemavu hususani wasioona wanauwezo wa kufanya shughuli kama watu wengine hivyo ni vyema jamiii ikaendela kushirikiana nao kwa usawa katika mambo ya maendeleo nchini.
Halikadhalika amebaisha kuwa bado kuna changamoto mbali mbali zinazotatiza kundi hilo, hususani kati suala la upatikanaji wa mikopo na wameomba mamlaka za wilaya, mkoa na wizara kwa ujumla kuwasaidia katika utatuzi wa changamoto hiyo kwa kuweka misingi imara ya usawa kwa watu watu.
Afisa wa watu wenye ulemavu wilaya ya kaskazin A Unguja Khamis Rashid Khamis amekiri bado watu wenye ulemavu wanachangamo katika suala la mikopo lakini kuna fungu Lao kutoka baraza la manispaa ambapo amawataka wafuate utaribu katika upatikanaji wa mikipo kama ya watu wengine na kuwahasa wanajamii kuwa watu wenye ulemavu wakiwezeshwa wanaweza kama watu wengine.
Katika kuhamasisha na kuunga mkono juhudi za watu wenye ulemavu, mwenyekiti wa chama cha CCM mkoa wa kaskazini Unguja Iddi Ali Ame alifanya harambee katika hafla hiyo na kupatikan shilingi laki nane na nusu zilizochangwa na viongozi, wageni na wananchi mbali mbali waliohudhuria hafla hiyo.
(Imeandikwa na Nishan Khamis na kuhaririwa na Ali, Khamis M)