Adhana FM

RC Kaskazini Unguja afanya ziara ya kushtukiza Hospitali ya Kivunge

1 June 2024, 12:19 pm

Na Nishan khamis, Kaskazin Unguja

Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Unguja Rashid Hadid Rashid amefanya ziara ya kustukiza katika hospital ya wilaya ya Kivunge kwa lengo na kusikiliza kero na changaomoto zinazowakabili wagonjwa na watendaji wa hospital hiyo.

Katika ziara hiyo Hadid amesema ameridhishwa na utoaji wa huduma katika hospital hiyo, licha ya uwepo wa changamoto kwa baadhi ya wafanyakazi kuchelewa kufika kazini, hali inayozorotesha upatikanaji wa huduma kwa wagonjwa katika hospital hiyo.

Hadid ametoa onyo kwa wafanyakazi wachelewaji na kisisitiza kuwa serikali ya mapinduzi ya zanzibar inaendelea kuimarisha miundonimbinu katika vituo vya afya kwa utoaji na upatikanaji wa huduma bora za kiafya nchini.

Halikadhalika amewasisitiza wananchi kuwa tabia ya kuvitumia vituo vya afya vilivyo karibu yao ili kupunguza msongamano katika hospital ya Kivunge.

Nae msadizi daktari dhamana wa hospital ya Kivunge, Tamimu Hamad Said amesema miongoni mwa sababu za kuchelewa kwa baadhi ya wafanyakazi ni changamoto za usafiri kwani wafanyakazi wengi wanaishi Mjini Magharibi.

Aidha dakitari Tamimu amewahimiza wananchi kuendelea kudumisha usafi wa mazingira ili kuepukana na maradhi mbali mbali ya mripuko katika jamiii.

Kwa upande wao baadhi ya wagonjwa wameelezea kufurahishwa na ziara hiyo, kwani imesaidia kusema kero zao na changaomoto zinazo jitokeza katika hospital, hivyo wameomba kuendelea kuimarishwa zaidi upatikanaji wa huduma kwa haraka za uhakika ili kuepusha vifo vya mama na mtoto katika mkoa wa Kaskazini Unguja.

Imeandikwa na Nishan Khamis na kuhaririwa na Ali, Khamis M.