Majadiliano baina na serikali na wadau ni suluhisho la changamoto za usafi wa mazingira.
2 October 2021, 9:48 am
Na Ali Khmais, Zanzibar
Majadiliano baina ya wadau na jamii ni njia muafaka ya kutatua changamoto katika masuala ya usafi wa mazingira ili kuiepusha jamii kukumbwa na maradhi ya mripuko. .
Katika majadiliano yaliyowaleta pamoja serikali na wadau, imebainishwa kuwa ili kuondoa changamoto zinazokwamisha juhudi za usafi wa mazingira, ni muhimu kutolewa elimu juu ya kuzangaa taka na hatari zake kwa binadamu na viumbe hai wenggine.
Afisa afya Kutoka wilaya ya magharib B Unguja, amesema kuwa, kutenga eneo maalumu la kukusanyia taka kabla ya kupelekwa jaa kuu la serikali ni jambo la dharura katika shehiya ya Mwembe Majogoo kutokana na wakazi wengi kutoa maoni yao kuhusu mahitaji ya kuwepo kwa eneo hilo kwa sasa.
Mjumbe Kutoka Iadara ya Kinga na mafunzo ya wizara ya afya, ustawi wa jamii, jinsia, wazee na watoto amesema kuwa jambo la muhimu kwa sasa ni kuazisha Mashindano ya usafi wa mazingira katika ngazi ya shehiya ambapo shehiya itakayoibuka mshindi kuwe na utaratibu wa kutolewa zawadi mbali mbali.
Aidha suala la kuweka kanuni juu ya udhibiti na usimamizi wa usafi katika ngazi ya shehiya litasaidia kuweka nidhamu kwa watu kwa nia ya kuilinda jamii ili isiathiriwe na magonjwa ya mripuko.
Kwa upande wake Mratibu wa Vikundi vya federation Zanzibar, Sadifa Othman Kaswela amesema wataongeza nguvu katika kuimarisha shughuli za vikundi katika wilaya ya magahrib B hususan eneo la Mwembe majogoo ili kusaidia juhudi za serekali katika kuondoa uchafu katika jamii.
Naye Sheha wa shehiya ya Mwembe majogoo amaesema kuwa tokea shirika la Centre for Community Initiatives ( CCI ) na Muungano wa vikundi vya federation Tanzania (TUPF) kuaza harakati za kukusanya taarifa zinazohusu masuala ya usafi wa mazingira katika shehiya za wilaya ya magharib B kuazia Aprili mwaka huu, wananchi wameanza kubadilika na amesisitiza taarifa hizo ziwe ni njia ya utatuzi wa changamoto mbali mbali katika jamii