Watu wenye ulemavu wa uziwi ni miongoni makundi yanayoishi kwenye dimbwi la umasikini Zanzibar
29 September 2021, 7:36 pm
Na mwandishi wetu, Wilaya Kusini Unguja.
Jumuiya Ya Viziwi Zanzibar Imesema Kundi Kubwa La Watu Wenye Ulemavu Wa Uziwi Liko Nyuma Kimaendeleo Hususan Vijijini.
Mwenyekiti Wa Jumuiya Viziwi Zanzibar Bi Asha Ali Haji Ameyaeleza Hayo Mara Baada Ya Kufanya Kazi Za Usafi Katika Hospitali Ya Wilaya Makunduchi Na Kazi Ya Utandazaji Wa Kifusi Katika Soko Jipya La Kijini Makunduchi Ikiwa Shamra Shamra Ya Kuelekea Kwenye Kilele Cha Maadhimisho Ya Wiki Ya Viziwi Duniani.
Amesema Licha Ya Serekali Na Taasisi Mbali Mbali Nchini Kuendelea Na Juhudi Za Kuwakomboa Watu Wenye Ulemavu Wa Uziwi Bado Jamii Haina Muamko Wa Kutosha Katika Kutetea Haki Zao Hivyo Amewashauri Wazazi Na Walezi Kuacha Tabia Ya Kuwaficha Watoto Wao Na Badala Yake Kuwashirikisha Katika Masuala Ya Kijamii Ikiwemo Kuwapatia Elimu Ya Lugha Za Alama .
Nae Kijana Mwenye Ulemavu Wa Uziwi Abdul Aziz Muhammed Mahfoudh Amesema Wakati Umefika Sasa Serekali Na Jamii Kuona Umuhimu Wa Kulipa Kipau Mbele Suala La Kujifunza Lugha Ya Alama Kwa Lengo La Kurahisisha Upatikanaji Wa Mawasiliano Ili Waweze Kuzifikia Fursa Mbali Mbali Nchini.
Akizungumza Kwa Niaba Ya Daktari Dhamana Wa Hospitali Ya Wilaya Makunduchi Daktari Amour Muhsin Burhan Ameishukuru Jumuiya Hiyo Kwa Hatua Yakeyakufanya Usafi Hospitalini Hapo Na Kuwataka Kuendelea Kushiriki Kikamilifu Katika Kazi Zinazohusiana Na Jamii Huku Akiiomba Jamii Kuthamini Juhudi Zao.
Wiki Ya Viziwi Husherehekewa Kila Mwaka Ifikapo Wiki Ya Mwisho Ya Mwezi Wa Septemba Na Kauli Mbiu Kwa Mwaka Huu Ni Sherehekea Ustawi Wa Jamii Ya Watu Wenye Ulemavu Kwa Maeneo Makuu Ya Lugha Ya Alama Na Tambua Uwepo Wa Historia Nzuri Ya Kupendeza Ya Watu Wenye Ulemavu Wa Uziwi .