Uvinza FM

Wanawake tupunguze maneno kwa waume zetu

9 March 2026, 10:09 pm

Picha ya Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto Wilaya ya Uvinza na Polisi Kata Inspekta Winfrida Joram akiwa katika kipindi cha kumekucha. Picha Alphonce Joseph

anapoanza kwenda huko inaweza kuwa sababu ya familia kutelekezwa na watoto kukosa huduma za Msingi

Na. Abdunuru Shafii

Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto Wilaya ya Uvinza na Polisi Kata Inspekta Winfrida Joram,  amewataka akina mama kutokuwa na maneno mengi kwa waume zao, kwani wakati mwingine maneno hayo yanawafanya wanaume kutopenda Nyumbani na wengine kutelekeza familia zao, jambo linaloathiri Malezi ya watoto hata kupelekwa kuongezeka kwa vitendo vya ukatili

Aidha Insp. Winfrida ameongeza kuwa, maneno yanapokuwa mengi yanaweza kumfanya baba asione sababu ya kuendelea kuwepo nyumbani na kuamua kwenda mtaani, au mahali kwingine ili kutafuta maisha yake binafsi na anapoanza kwenda huko inaweza kuwa sababu ya familia kutelekezwa na watoto kukosa huduma za Msingi kama vile Chakula, Elimu, matibabu na Malezi bora

sauti ya Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto Wilaya ya Uvinza na Polisi Kata Inspekta Winfrida Joram

Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Ruchugi, kata ya Uvinza Wilayani Uvinza Mch. Gidion Daudi Lumanagaze, akieleza sababu za wazazi kutelekeza familia na hasara zake kwa watoto kihuduma akisema kuwa mtu asiyeitunza Familia yake anakuwa ameikana Imani.

sauti ya Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Ruchugi, kata ya Uvinza Wilayani Uvinza Mch. Gidion Daudi Lumanagaze

Nae Imamu wa Msikiti Maamuru, kijiji na kata ya Uvinza Wilayani Uvinza Shekh. Madua Ramadhani, ameeleza namna migogoro ya kifamilia na wazazi kutotimiza wajibu wao vizuri, kunavyoleta madhara kwa watoto hasa mmomonyoko wa maadili na hata vitendo vya ukatili katika jamii

sauti ya Imamu wa Msikiti Maamuru, kijiji na kata ya Uvinza Wilayani Uvinza Shekh. Madua Ramadhani