Uvinza FM
Uvinza FM
3 February 2026, 1:21 am

Naomba mkatoe elimu kwa wananchi na kuhakikisha wanaelewa mkakati wa serikali wa kutoa bima ya afya kwa wote
Na. Emmanual Kamangu
Wanufaika kaya masikini TASAF elfu 66800 mkoani kigoma Kunufaika bure na bima ya afya kwa wote ikiwa ni mpango wa serikali kuendelea kutoa huduma bora za afya kwa kaya ambazo hazijiwezi.
Mkuu wa wilaya ya kasulu Kanal Isack Mwakisu akizungumza na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya kasulu amewaomba kutoa elimu kwa wananchi kuhakikisha wanaelewa mkakati wa serikali wa kutoa bima ya afya kwa wote zoezi ambalo linategewa kuanza bure kwa kaya masikini Tasaf.

Aidha Kanal Mwakisu amesema kuwa baada ya zoezi hilo kukamilika kwa kaya masikini Tasaf litahamia kwa jamii nzima ambapo wanafamilia sita watanufaika na bima ya afya kwa kiwango cha Tsh laki moja na elfu hamsini pekee na kuwasaidia kupata huduma bure za afya kuanzia ngazi ya zahanati na kuendelea.
Fabiano Dangi Doragi ni diwani wa kata ya rusesa ambaye ni mmoja wa madiwani ambao wameshiriki mkutano huo amepongeza serikali kwa kuja na mpango wa bima ya afya kwa wote jambo litakalosaidia kwa kiasi kikubwa wananchi kupata matibabu kwa wakati na kuimalisha afya zao.