Uvinza FM

Tanzania yaweka kipaumbele jinsia na tabianchi COP30

10 November 2025, 10:18 am

Picha ya bango la mkutano wa mabadiliko ya tabianchi, Picha kutoka mtandaoni

Wadau wa maendeleo wanaaswa kuwekeza katika elimu, teknolojia rafiki kwa mazingira, na miradi ya kiuchumi itakayowawezesha wanawake kuwa sehemu ya suluhisho la mabadiliko ya tabianchi.

Na Abdunuru Shafii

Wanawake wa wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma wameendelea kukabiliwa na athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi ambazo zimekuwa zikiathiri maisha yao ya kila siku, hasa katika upatikanaji wa maji, chakula na kipato. Hali hiyo imeibua mjadala mpana kuhusu umuhimu wa kujumuishwa kwa sauti za wanawake katika ajenda za mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi (COP 30) unaotarajiwa kufanyika nchini Brazil, ambapo masuala ya usawa wa kijinsia na mazingira yanatarajiwa kupewa kipaumbele.

Baadhi ya wanawake wa Uvinza wanasema mabadiliko ya tabianchi yameharibu mavuno na kuongeza ugumu wa maisha vijijini huku hali ya hewa isiyotabirika imeathiri uzalishaji wa chakula na kulazimisha wanawake kutumia muda mwingi kutafuta maji na kupanda kwa bei ya bidhaa za chakula kumechangia ongezeko la changamoto za kiuchumi kwa wanawake.

Kwa upande wake, Mtaalamu wa Mazingira kutoka jays and n general supplies and consult company ltd), bwana Josiah Sendwa, amesema mabadiliko ya tabianchi ni mabadiliko ya muda mrefu ya hali ya hewa yanayosababishwa na ongezeko la gesi joto angani, hali inayosababisha ukame, mafuriko, na upungufu wa maji.

Sauti 1 ya Mtaalamu wa Mazingira kutoka Jays and N general supplies and consult company ltd), bwana Josiah Sendwa

Ameongeza kuwa serikali na wadau wa maendeleo wanapaswa kuwekeza katika elimu, teknolojia rafiki kwa mazingira, na miradi ya kiuchumi itakayowawezesha wanawake kuwa sehemu ya suluhisho la mabadiliko ya tabianchi.

Sauti 2 ya Mtaalamu wa Mazingira kutoka Jays and N general supplies and consult company ltd), bwana Josiah Sendwa