Uvinza FM

Wazee ni tunu tuwajali na kuwatunza

2 October 2025, 7:11 pm

Wazee wakipata elimu katika maadhimisho ya kilele siku ya wazee duniani kata ya nguruka.

Wananchi wametakiwa kushilikiana na serikali katika kuibua changamoto ya unyanyasaji wa kijinsia unaofanyika kwa wazee.

Na Dunia Stephano

Kaimu mtendaji ambaye pia ni Afisa maendeleo wa kata ya nguruka wilaya ya Uvinza Sarafina jonijo mapasi amewataka wananchi kushilikiana na serikali katika kuibua changamoto ya unyanyasaji wa kijinsia unaofanyika kwa wazee.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wazee katika kilele cha  maadhimisho ya siku  ya wazee duniani iliyofanyika nguruka iliyokuwa na kaulimbiu isemayo wazee tushiriki uchaguzi kwa ustawi wa jamii.

Sauti mtendaji kata

 Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii  kata ya nguruka  Miraji pazi ameyataka mashirika ya serikali na yale yasio ya kiserikali kuendelea kushirikiana kwa pamoja kwani ushirikiano ndio nguzo na heshima katika kuleta utu.

Afisa ustawi wa jamii  kata ya nguruka  Miraji pazi akitoa Elimu wakati wa maadhimisha kata ya nguruka

Sauti afisa ustawi

Aidha afisa tabibu kutoka kituo cha afya nguruka Ado Crispini mapunda amewataka wazee  kuhudhuria kliniki kwa ajiiri ya kuendelea na kupima magonjwa yasiyoyakuambukizwa ikiwemo magonjwa ya moyo na shinikizo la damu.

Sauti afisa tabibu

Kwa upande wao wazee waliohudhuria tukio hilo wamesema kuwa vijana wanapaswa kuwavumilia wazee wao na wawaheshimu  kutokana na uzee wao .

Sauti wazee

Ikumbukwe kuwa tukio hilo la siku ya wazee dunia katika kata nguruka limehudhuriwa na watu mbalimbali ambao wamefanikisha shuguli ikiwemo uvinza paralegal foundation,nguruka development agency pamoja na SMAUJATA Uvinza.