Uvinza FM
Uvinza FM
1 October 2025, 11:40 am

“Nitahakikisha naishauri serikali kurekebisha sheria na sera rafiki za uwekezaji ili vijana wanaosoma wapate ajira rasmi.” Eliya Mahwa
Na. Theresia Damasi
Mgombea wa ubunge jimbo la Kigoma Kusini kwa tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma CHAUMA BW. Eliya Mahwa amesema kuwa atarudisha hadhi na heshima ya elimu endapo atapata ridhaa kwa wananchi kuongoza jimbo hilo.
Amesema hayo kwenye kipindi cha kumekucha na uvinza fm kuwa atahakikisha anaishauri serikali kurekebisha sheria na sera rafiki za uwekezaji ili vijana wanaosoma wapate ajira rasmi huku ambao hawajapata elimu waweze kujiajiri wenyewe .
Sanjari na hayo Mgombea huyo amesema kuwa migogoro mingi ya ardhi inatokana na wingi wa watu na mifugo ambapo michoro ya ardhi imechorwa muda mrefu hivyo kuna umuhimu wa serikali kutambua ongezeko na uhitaji wa ardhi pamoja na kupitia upya mipaka kwa kurasimisha kutokana na mahitaji ya sasa.
Aidha Mgombea Mahwa amesema wananchi wa jimbo la Kigoma Kusini wamepata tabu ya kukosa maji safi na salama kwa mda mrefu, ambapo atahakikisha anaenda kuweka miundombinu kwa siku 90 pale anapochaguliwa kuwa mbunge.
Pamoja na hayo ila ya chama cha ukombozi {CHAUMA}kwa mwaka 2025 hadi 2030 inasema itasimamia Madaraka ya umma,Maadili ya uongozi, Lishe kwa wote, Utawala Bora,Ardhi maendeleo ya watu na Elimu Bora .