Uvinza FM
Uvinza FM
11 August 2025, 8:33 pm

Kikundi cha akina mama wajasiriamali kajeje kata ya ilagala wameeleza mafanikio ya miradi mitatu 3 ikiwemo kulima pamba, kununua nyumba na kulima mbogamboga ambayo imeondoa adhaa ya umasikini katika familia zao mara baada ya kupata mkopo wa milion kumi {10}.
Na Theresia Damasi
Kikundi cha wanawake wanaojishughulisha na shughuli za ujasiriamali katika kata ya ilagala, kijiji cha kajeje halmashauri ya wilaya ya uvinza wameishukuru serikali kwa kuwawezesha kupata mkopo wa asilimia 10 ambao unatolewa na halmashauri bila ya riba ambapo wameeleza mafanikio ikiwemo kuendeleza miradi mbalimbali ikiwemo kilimo.
Akizungumza na uvinza fm redio mwenyekiti wa kikundi cha akina mama wajasiriamali kajeje Bi. Nzeimana Zaazura ameeleza mafanikio ya miradi 3 ikiwemo kulima pamba, kununua nyumba na kulima mbogamboga ambayo imeondoa adhaa ya umasikini katika familia zao.

Sauti ya M/Kiti Nzeimana
Bi. Nzeimana amesema umoja ni nguvu utengani ni udhaifu ambapo amesema toka walipopata mkopo wa asilimia 10 changamoto za kwenye ndoa zilizokuwa zinajitokeza baina akina baba na akina mama kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi zimepungua.
Sauti M/Kiti Nzeimana
Aidha Bi.Nzeimana amewashauri akinamama na vijana waunde vikundi kwa lengo la kuchukua mkopo unaotolewa na serikali bila riba ili wajiendeleze kiuchumi na kuondokana na umasikini katika jamii.
Sauti ya M/Kiti Nzeimana
Bi.Anjela Chakupewa ni mmoja ya mwanakikundi cha ujasiriamali kajeje ambapo amesema kupitia mkopo waliopewa na serikali umemnufaisha kwa kusomesha watoto na kujiinua kiuchumi ambapo hapo mwanzo alikuwa anafanya shughuli ngumu ambazo malipo yake ni madogo.
Sauti ya Bi. Anjela Chakupewa
Kwa upande wake mkuu wa Idara ya maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya uvinza Bw. Godfrey Nkuba amekipongeza kikundi cha akina mama kajeje kwa kufanikisha malengo yao toka walipochukua mkopo kwa kuendesha miradi mbalimbali ambapo amesema wanastahili kupata mkopo mwingine kwa ajili ya kujiinua kiuchumi Zaidi.

Sauti ya Bw. Nkuba
Aidha Bw.Nkuba amesema sababu mojawapo ya wanawake kufanyiwa ukatili ni kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumu hasa ya kipato na kushindwa kumiliki mali ambapo takwimu zinaonesha kupungua kwa matukio ya ukatili huku jitihada za uelimishaji zikiendelea kutolewa.
Sauti ya Bw.Nkuba
Hata hivyo mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na serikali katika kila halmashauri bila riba ni kwa lengo la kuwainua akinamama, vijana na makundi maalumu kujikwamua kiuchumi na kutokomeza ukatili katika ndoa .
