Uvinza FM

Uvinza wahimizwa kuacha ukatili wa ulawiti, ubakaji

1 August 2025, 1:46 pm

Wanafunzi wa shule ya msingi wa ilagala pamoja na timu ya uelimishaji wakiwa katika maandano kupinga masuala ya ukatili wa kijinsia kwa watoto.

Jamii wilayani Uvinza imetakiwa kuacha matukio ya kikatili hasa ulawiti na ubakaji kwa watoto na wanawake ili jamii iwe salama huku wakitakiwa kujikita katika maendeleo.

Na Theresia Damasi

Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia na Watoto wakishirikiana na Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya Uvinza mkoani Kigoma pamoja na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) wamewataka wananchi kuacha matukio ya ukatili ikiwemo ubakiji na ulawiti kwa watoto na wanawake ili jamii iwe salama.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Ilagala katika mkutano wa hadhara, mkuu wa dawati la jinsia na watoto Ispekta Winfrida Joram amesema mtu anapofanyiwa ukatili anatakiwa kuripoti mapema kituoni bila kupoteza ushahidi.

Mkuu wa dawati la jinsia na watoto halmashauri ya uvinza Winfrida Joram akitoa elimu kwa wananchi wa kata ya ilagala juu ya masuala ya ukatili.
Sauti ya Inspekta Winfrida

Kwa upande wake Christopher Mtabazi Afisa maendeleo ya jamii ameeleza namna ya ukatili wa kisaikolojia unavyowaathiri watoto na wanawake ikiwemo matusi.

Afisa maendeleo ya jamii Christopher Mtabazi akitoa elimu kwa wananchi juu ya athari za ukatili
Sauti ya afisa maendeleo

 Kadhalika Winfrida kutoka msaada wa kisheria halmashauri wilaya ya Uvinza ameeleza namna ya wazazi ama walezi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwalea watoto katika maadili adilifu katika jamii.

Sauti Winfrida msaada wa kisheria

Naye Mkuu wa idara ya maendeleo wa halmashauri ya wilaya ya Uvinza Godfrey Nkuba ametoa zawadi kwa watoto waliofanikiwa kujibu maswali ya uelewa katika somo la ukatili huku akiwataka wazazi kuacha mara moja tabia ya kuwatumikisha watoto mpaka usiku badala yake watumie mda huo kuwafuza maadili mema .

Mmoja ya wanafunzi akipokea zawadi kutoka wa maafisa maendeleo wanaotoa elimu ya kupinga ukatili .
Sauti ya Afisa maendeleo Godfrey Nkuba

Hata hivyo timu hiyo ya  uelimishaji kutoka halmashauri ya wilaya ya uvinza ikiongozwa na mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii wametembelea shule ya msingi Ilagala ambapo wamefanya maadamano na wanafunzi wa shule hiyo huku wakiwapa elimu juu ya  athari mbalimbali za vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto na namna watoto hao wanaweza kusaidia kupambana na vitendo vya ukatili kwa kutoa taarifa ya matukio yanayotokea kwenye ngazi na mamlaka zinazohusika katika maeneo yao.