Uvinza FM
Uvinza FM
9 July 2025, 1:50 pm

Zaidi ya vyandarua elfu 16 vitagawiwa kwa wananchi wa Kata ya Uvinza kama sehemu ya juhudi za kuendelea kutokomeza ugonjwa hatari wa malaria katika Wilaya ya Uvinza.
Na Abdunuru Shafii
Wananchi wa kata ya uvinza wilaya ya uvinza wamepokea vyandarua kwa kila kaya hii ikiwa ni mkakati wa serikali wa kutokomeza malaria katika wilaya ya uvinza na mkoa wa kigoma kwa ujumla.
Zoezi hilo la kugawa Vyandarua Zaidi ya elfu 16 katika kata ya uvinza limeanza rasmi leo 08/07/2025 likiongozwa na katibu tawala wilaya ya uvinza Ndg. James Mkumbo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya uvinza Dinnah Mathaman.
Mkumbo amewataka wananchi wanaochukua vyandarua na kuhakikisha wanavitumia katika matumizi sahahi na sio kuvitumia kufugia mifugo na kupandia mazao ili kutokomeza malaria.
Pia amewataka wananchi kuachana na dhana potofu ambazo zimekuwa zikisambaa mtaani na kuhakikisha tunawaamini wataalamu wetu si vinginevyo.
Nao wananchi wa kata ya uvinza wameahidi kuhakikisha wanatumia vyandarua kwa usahihi ili kuendelea kujikinga na ugonjwa hatari wa maralia