Uvinza FM

Upasuaji wa nyonga wafanyika kwa mara ya kwanza mkoani Kigoma

31 May 2025, 9:48 pm

Madakitari Bingwa wakifanya upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma (picha na sprian)

Mara nyingi huduma hizi ninapatikana katika hospitali kubwa za kanda lakini leo tumefanikiwa kufanya upasuaji huu mkubwa hapa, ni upasuaji wa kwanza hapa Maweni.

Na Abdunuru Shafii

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma imetoa huduma ya upasuaji kwa mgonjwa mwenye tatizo la nyonga kwa mara ya kwanza ikiwa ni siku ya tano ya kambi ya matibabu ya kibingwa katika hospitali hiyo.

Akizungumza Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali Dk. Joseph Nangawe amesema wananchi hawanabudi kufika kupata huduma hiyo kwasababu wataalamu wako makini pia mgonjwa uangaliwa kwa umakini kuhakikisha anapata huduma bora.

Pia Dk. Nangawe amesema kuwa jitihada za Serikali ya awamu ya sita chini ya Mh. Dk. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kwa kuwapeleka madaktri Bingwa na Bobezi katika hospitali za kanda Pamoja na hospitali za rufaa ambao wanasaidia sana kutoa huduma kwa wananchi.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali Dk. Joseph Nangawe

Nae Dk. Wilson Masanja ambaye ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya mifupa kutoka Hospitali ya Kanda Bugando Mwanza amesema, katika kambi hii ya siku tano huduma ya kumbadilishia nyonga mgonjwa ambaye amesumbuliwa na tatizo la nyonga kwa muda mrefu imefanyika huku akitoa wito kwa wananchi kutumia Hospitali ya Maweni kupata huduma hizo kwani kuzifata mbali ni gharama kubwa.

Dk. Masanja ameendelea kusema kuwa upasuaji ambao umefanyika leo umefanyika kwa asilimia 100 ambapo matibabu hayo hamefanyika ili kumtoa mgonjwa kitandani hivyo atarudi katika haliyake ya kawaida atatembea.

Dk. Wilson Masanja Daktari Bingwa wa magonjwa ya mifupa Hospitali ya Bugando Mwanza