Uvinza FM

Wananchi waaswa kula vyakula vya kunde

11 February 2025, 4:52 pm

Picha ya baadhi ya Mikunde katika siku ya maadhimisho ya Mikunde.Picha na Theresia Damas.

Wananchi wametakiwa kujenga tabia ya kula vyakula vya jamii ya mikunde kwa lengo la kuboresha Afya.

Na Theresia Damas

Ikiwa ni Maadhimisho ya siku ya mikunde Duniani, wananchi wametakiwa kujenga tabia ya kula vyakula jamii ya mikunde kwa lengo la kuboresha Afya na kukuza uchumi kupitia mazao ya mimea ya jamii hiyo.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya soko la Lugufu lililopo makao makuu ya wilaya katika Kijiji cha Ruchugi kata ya Uvinza.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza Ndg. Acland.Picha na Theresia Damas.

Mgeni Maalum katika maadhimisho hayo ni kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza Ndg. Acland Kambili ambapo amewataka wananchi kuacha tabia ya kula maharage kama mazoea, ametoa rai kula mbaazi, choroko na kunde ili kuwa na jamii yenye Afya nzuri.

Sauti ya kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza Ndg. Acland kambili.

Afisa Kilimo katika halmashauri ya wilaya ya Uvinza Bi.Toligwe Kaisi.Picha na Theresia Damas.

Naye Toligwe Kaisi ambaye ni Afisa kilimo katika Halmashauri ya wilaya ya Uvinza amesema katika kuadhimisha siku ya  mikunde duniani wananchi wafahamu umuhimu wa kulima mazao hayo na kula kwani yatawasaidia katika kuboresha afya na kuepukana magonjwa mbalimbali ikiwemo kisukari.

Sauti ya Afisa Kilimo katika Halmashauri ya wilaya ya Uvinza Bi.Toligwe Kaisi.

Wananchi waliohudhuria maadhimisho ya Mikunde.Picha na Theresia Damas.

Nao wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo wamesema wamefaidika na mafunzo mbalimbali yanayotelewa na FAO katika halmashauri hiyo, ambapo wameiomba serikali kuwatafutia masoko ya kuuzia mazao yao.

Sauti za wananchi.

Ikumbukwe kwamba Maadhimisho haya yamefanyika kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la chakula Duniani (FAO) kwa kutoa mafunzo kwa wakulima kwa lengo la kufanya kilimo chenye tija na kuweza kuimarika kiuchumi.