

31 January 2025, 3:47 pm
Wananchi wilayani Uvinza wameaswa kuandika wosia na kuratibu mali walizonazo ili kuepukana na changamoto zisizo na ulazima.
Na Linda Dismas
Ikiwa ni wiki ya sheria duniani, wananchi wilayani Uvinza wameaswa kuandika wosia na kuratibu mali walizonazo ili kuondoa utata unaojitokeza katika familia pindi wahusika wanapopata changamoto.
Hayo yameelezwa na Frank Japhet Mtega hakimu mkazi mahakama ya Halmashauri ya Uvinza wakati akizungumza na radio Uvinza fm ambapo amesema kuna sheria kadhaa zinazotumika kuendesha maswala mazima ya mirathi.
Hakimu huyo ameendelea kusema kuwa kila sheria inatokana na desturi mbalimbali nchini Tanzania ikiwemo sheria ya Kiislamu na kwamba sheria hii itawahusu watanzania wote endapo itadhihirika kwamba wameachana na mila na desturi zao.
Hata hivyo hakimu Frank Japhet Mtega amesema baadhi ya sheria bado zinawakandamiza wanawake na watoto wa kike, hivyo kupelekea kukiuka haki za binadamu.
Aidha amewaomba wananchi kujitokeza katika maeneo mbalimbali ya kutolea msaada wa kisheria ili kupata haki zao za msingi.