Uvinza FM

Wiki ya sheria wananchi mjitokeze kupata elimu

28 January 2025, 8:55 pm

Picha ya Misana Mganga Majula akiwa anafanya majadiliano na uvinza fm.Picha na Linda Dismas.

Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya uvinza, amewaasa wananchi kujitokeza kushiriki ili kupata elimu ya masuala mbalimbali yanayohusu sheria.

Na Theresia Damasi

Wananchi wilayani Uvinza mkoani kigoma wametakiwa kuchangamkia fursa ya kupata haki zao za msingi kwa kupata elimu ya sheria ili kuepuka kuvunja sheria zilizowekwa.

Hayo yameelezwa na Misana Mganga Majula Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya uvinza, katika kipindi cha kumekucha ikiwa ni siku ya nne toka kuzinduliwa kwa wiki ya sheria katika wilaya ya Uvinza.

Ambapo Majula amesema katika wiki ya sheria wanatoa Elimu bure ya sheria na msaada wa kisheria kwa wananchi hivyo wananchi wajitokeze katika maeneo yakiwemo Shule ya sekondari Mganza, Shule ya msingi Muungano, Rugufu, pamoja na Shule ya msingi Ilagala.

Sauti ya Misana Mganga Majula.

Aidha Hakimu Mfawidhi huyo amesema kutokujua sheria kwa wananchi isiwe kigezo cha wao kuvunja sheria na taratibu zilizowekwa bali katika wiki hii ya sheria wafuatilie kwa karibu katika maeneo yao ili kupata elimu.

Sauti ya Misana Majula.

Ikumbukwe kuwa hii ni siku ya nne toka wiki ya sheria ilipozinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi. Dinnah Mathaman tarehe 25 januari 2025 ambapo kauli mbiu ya mwaka 2025 inasema nafasi ya taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo makuu ya dira ya taifa ya maendeleo.