Mazingira machafu migahawani yanavyohatarisha maisha ya watu
25 January 2025, 5:04 pm
Mamantilie wakiendelea na shughuli zao za kupika chakula. Picha kutoka maktaba
Walaji wa vyakula vya migahawani walia na changamoto wanazozipata kutokana na vyakula hivyo.
Na Kelvin Mambaga
Wananchi wa wilaya ya uvinza mkoani kigoma wameeleza namna ambavyo mazingira ya migahawani sii rafiki kwa afya zao.
Wameyasema hayo wakati Wakizungumza na uvinza fm na kuelezea kuwa kuna baadhi ya wahudumu wa migahawa hawazingazii kanuni za usafi wa vyakula hali inayowapelekea wao kama walaji kupata changamoto za kiafya.
Nae dk. David samsoni kutoka hosptali ya wilaya uvinza amebainisha kuwa vyakula ambavyo sii salama kwa afya ya mlaji ni vyakula visivyo zingatia usafi katika uandaaji.
Dk davidi ameongeza na kusema kuwa ulaji wa vyakula visivyo na visafi unasababisha magonjwa hatari kama vile kipindupindu kuhara na magonjwa mengi ya tumbo.