Uvinza FM

Watumishi saba wa idara ya Afya kukatwa asilimia 15 ya mshahara wao

20 November 2024, 2:19 pm

Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya kibondo picha na Emmanuel Kamangu

Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya kibondo wamefanya kikao cha utekelezaji wa shughuli za maendeleo za kata na kulidhia kuwakata asilimia 15 ya mshahara watumishi saba wa idara ya afya

Na Emmanuel Kamangu

Baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya kibondo limeadhimia watumishi saba wa idara ya Afya kukatwa asilimia 15 ya mshahara wao kwa kipindi cha miaka mitatu na kurudisha fedha zaidi ya milioni 70 walizo hjumu serikali kwa kuuza dawa na vifaa tiba kinyume na utaratibu.

Mara baada ya baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya kibondo mkoani kigoma kutoa adhabu hiyo, uvinza FM imezungunza na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo bwana Habili Charles Maseke.

Sauti ya Habili Charles Maseke

Nao baadhi ya wakazi wa wilaya ya kibondo wametoa maoni haya baada ya sakata hilo ambalo limeibua hisia kubwa miongoni mwa wananchi wengi

Sauti za wananchi wilaya ya kibondo

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kibondo bwana Diocles M. Rutema amesema haya juu ya adhabu iliyo tolewa na madiwani