Uvinza FM

Wanawake watakiwa kuunda vikundi ili wapate mikopo ya Serikali

24/11/2021, 4:09 pm

Wanawake wajasiriamali Mkoani Kigoma wametakiwa kuunda vikundi, ili waweze kupatiwa mikopo na Serikali ili kuweza  kendeleza shughuli zao na kujikomboa kiuchumi

Hayo yamesemwa na Afisa Maendeleo Halmashauri ya wilaya ya Kigoma ZILIPA KISONZELA mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya kuwawezesha wanawake kutoka kaya Masikini ili waweze kujikomboa kiuchumi yaliyoratibiwa na kituo cha huduma ya Mtoto Kanisa la Angilikana Mwandiga wakishirikiana na Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo SIDO Mkoa wa Kigoma

Sauti ya afisa maendeleo

Kwa upande wake Mratibu wa huduma ya mtoto kanisa la Angilikana Mwandiga LILIAN MAGESA Ameeleza sababu ya wao kutoa mafunzo hayo, huku  Mkufunzi wa usindikaji wa vyakula mbalimbali kutoka Shirika  la SIDO Mkoa wa Kigoma ATUKETILE MWASALEMBA, akataja baadhi ya mafanikio ambayo wameyapata tangu waanze kutoa mafunzo kwa akina Mama wajasiriamali

Sauti ya mratibu

Nao baadhi ya wanawake wajasiriamali ambao wamepatiwa mafunzo hayo, wamesema mafunzo hayo yatakuwa msaada mkubwa kwao, huku wakikiri kuwa wataunda vikundi ili iwe rahisi kwao kupata mikopo kutoka kwa Serikali.

Sauti ya wajasiriamali