Shilingi bilioni 2 kujenga vyumba vya madarasa
19 November 2021, 7:13 pm
Na,Glory Paschal
Wananchi Manispaa ya Kigoma Ujiji wametakiwa kushiriki kikamilifu katika zoezi la Ujenzi wa vyumba 48 vya madarasa, ambavyo vinatakiwa kukamili ndani ya siku 45
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma ESTER MAHAWE , akizungumza na wananchi wa kata ya Lusimbi Manispaa ya Kigoma Ujiji, katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa vyumba vya Madarasa amesema ushirikiano baina ya serikali na wananchi utasaidia kukamilisha ujenzii huo kwa wakati
Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji waliokuwepo katika hafla hiyo, akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ATHUMAN MSABILA wamesema watasimamia zoezi hilo kwa uaminifu
Nao baadhi ya wananchi Manispaa ya Kigoma Ujiji, wameshukuru Serikali kuwa na mpango huo wa ujenzi wa vyumba vya madarasa, huku wakieleza kuwa watashiriki kikamilifu katika ujenzi wa vyumba hivyo vya Madarasa
Kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwa Maana ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na Kigoma Vijijini, kwa ujumla wamepokea kiasi cha zaidi ya Shilingi Bilioni 2 kwa ajiri ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa kwa baadhi ya Shule za Sekondari.